TANZANIA NA IFC ZAJADILI USHIRIKIANO WA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI KWA MAENDELEO YA NCHI

TANZANIA NA IFC ZAJADILI USHIRIKIANO WA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI KWA MAENDELEO YA NCHI
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati akiongoza kikao na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika Mashariki, ukiongozwa na Mkurugenzi wake, Bi. Mary Porter Peschka, baada ya kukutana na kuzungumza katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050) . Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam Serikali ya Tanzania imerejea tena dhamira yake ya kushirikiana kwa karibu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha Mpango wa Taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (DIRA 2050). Akizungumza katika kikao na Mkurugenzi wa IFC Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Mary Porter Peschka, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M…