TANZANIA NA AUSTRIA KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA AFYA NA ELIMU
TANZANIA NA AUSTRIA KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA AFYA NA ELIMU Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kufurahishwa na ushirikiano wa kimatibabu kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha Tiba cha Vienna, huku ikikaribisha upanuzi wa ushirikiano huo katika taasisi nyingine za kibobezi ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), kwa lengo la kuboresha huduma za afya nchini. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya nje, Mhe. Ngwaru Maghembe (Mb), akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), katika mazungumzo ya kidiplomasia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria anayeshughulikia masuala ya kisiasa, Mhe. Balozi Dkt. Hannah Liko, yaliyofanyika Machi 24, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Maghembe amepongeza mchango wa Austria katika sekta ya elimu, ikiwemo utoaji wa mikopo yenye masharti nafu…