SHEIKH KABEKE AWAHIMIZA WAISLAMU KUDUMISHA AMANI, UMOJA NA UCHUMI HALALI

SHEIKH KABEKE AWAHIMIZA WAISLAMU KUDUMISHA AMANI, UMOJA NA UCHUMI HALALI
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhji Hasani Kabeke, akizungumza na maelfu ya waumini wa Kiislamu waliofurika kuswali Sala ya Idd El Fitri, kwenye Uwanja wa Nyamagana, leo. Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhji Hasani Kabeke, akiongoza  maelfu ya waumini wa Kiislamu waliofurika  kwenye Uwanja wa Nyamagana, kuswali  Sala ya Idd El Fitri, leo. Waumin wa Kiislamu, wakiswali Sala ya Idd El Fitri kimkoa, katika Uwanja wa Nyamagana, leo (Picha na Baltazar Mashaka) …………. NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA Waislamu mkoani Mwanza wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano katika jamii, huku wakihimizwa kuendeleza matendo mema waliyoyafanya katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Miongoni mwa matendo hayo ni pamoja na kulipa zaka na kuyajali makundi yenye uhitaji, hususan yatima, ili kuimarisha ustawi wa kijamii na mshikamano wa kitaifa. Wito huo ulitolewa leo na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke, baada ya Sala ya Idd El Fitri iliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Nyamagana,  akisisitiza kuwa amani ni msingi …