Serikali Yathibitisha Uhakika wa Upatikanaji wa Mafuta Nchini kwa Kipindi cha Miezi Mitatu

Serikali Yathibitisha Uhakika wa Upatikanaji wa Mafuta Nchini kwa Kipindi cha Miezi Mitatu
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeeleza kuwa hali ya upatikanaji wa mafuta nchini bado ni shwari, huku bei zikiwa himilivu, ambapo mafuta yaliyopo yanatosheleza kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, wakati akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na uhaba wa mafuta duniani uliotokana na vita inayoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Dkt. Mataragio amesema: “Mafuta yaliyopo nchini kwenye matenki, Petrol tuna lita 95,256,342; mafuta ya petrol yaliyowasili nchini ni lita 1,466,337; mafuta yaliyopo njiani kwenye meli ni lita 138,737,332. Hivyo, jumla ya mafuta ya Petrol yatakayokuwepo ni lita 380,677,011, na yanatosha kwa matumizi ya siku 61.” Ameongeza kuwa kuna mikataba ya mafuta iliyoingiwa na mzabuni yenye jumla ya lita 183,500,450 ambayo yatafika nchini mwezi wa…