Serikali Yajipanga Kuongeza Ushindani wa Bidhaa za Wanawake Kimataifa
Serikali Yajipanga Kuongeza Ushindani wa Bidhaa za Wanawake Kimataifa
Na Mwandishi Wetu SERIKALI inaendelea kujipanga kutunga sheria jumuishi zitakazoshirikisha sekta binafsi kwa lengo la kuimarisha uwezo wa wanawake katika uzalishaji na utengenezaji wa bidhaa zenye ubora na ushindani katika soko la kimataifa. Akizungumza Machi 28, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema hatua hiyo inalenga kuwapa wanawake mazingira bora ya uzalishaji na biashara ili waweze kushindana katika masoko ya kikanda na kimataifa. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kujenga uchumi jumuishi unaowashirikisha wanawake na vijana kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Kapinga alisema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kutenga asilimia 30 ya zabuni za manunuzi ya umma kwa makundi maalum, yakiwemo wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum, hatua inayosaidia kukuza biashara na kuongeza kipato kwa makundi hayo. Alitoa kauli hiyo katika maadhim…