SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA VYAKULA VYA ASILI KUIMARISHA AFYA NA KUZUIA MAGONJWA
SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA VYAKULA VYA ASILI KUIMARISHA AFYA NA KUZUIA MAGONJWA
Na Elimu ya Afya kwa Umma SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewahimiza Watanzania kurejea katika matumizi ya vyakula vya asili kama sehemu muhimu ya kujenga afya bora, kuzuia magonjwa, na kusaidia matibabu kwa njia salama na endelevu. Akizungumza jijini Dodoma katika Mkutano wa Waziri wa Afya na wataalam wa tiba asili, Mkurugenzi wa Huduma za Uhamasishaji wa Afya (Elimu ya Afya kwa Umma), Dkt. Rahma Ahmed Hingora, amesema vyakula vya asili vina mchango mkubwa katika kuimarisha afya ya mwili na vinaweza kutumika kama sehemu ya kinga na tiba iwapo vitatumika kwa usahihi. “Tunapaswa kurudisha utamaduni wa kula vyakula vya asili kama maboga, ubuyu na vyakula vingine vinavyopatikana katika mazingira yetu. Hivi ni vyakula vyenye virutubishi muhimu vinavyosaidia kuimarisha kinga ya mwili na afya kwa ujumla,” amesema Dkt. Hingora. Amebainisha kuwa kumekuwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha ambapo jamii imekuwa ikipuuza vyakula vya asili na kuelekea zaidi katika matumizi ya vyakula vilivyosindikwa,…