SERIKALI INABORESHA MIUNDOMBINU ILI MTOTO WA KITANZANIA APATE HAKI YAKE YA MSINGI YA ELIMU BORA - PROF. SHEMDOE

SERIKALI INABORESHA MIUNDOMBINU ILI MTOTO WA KITANZANIA APATE HAKI YAKE YA MSINGI YA ELIMU BORA - PROF. SHEMDOE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inaendelea kusimamia uboreshwaji wa miundombinu ya elimu nchini, ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata haki yake ya msingi ya elimu bora katika mazingira mazuri na rafiki ya ujifunzaji na ufundishwaji.  Prof. Shemdoe amesema, kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Msingi iliyopewa jina la Profesa Riziki Shemdoe ni sehemu ya utekelezaji wa azma hiyo ya Serikali ya kumuwezesha mtoto wa kitanzania kupata haki yake ya msingi ya elimu bora. Prof. Shemdoe amesema hayo leo Machi 22, 2026 akiwa katika Kata ya Ngwelo wilayani Lushoto, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Shule hiyo Mpya ya Awali na Msingi ya Profesa Riziki Shemdoe iliyojengwa katika Jimbo la Lushoto, Tarafa ya Mlola, Kata ya Ngwelo, Kijiji cha Kihitu. Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, ujenzi wa shule hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi pamoja na maelekezo ya Mhe. R…