RAIS SAMIA MSIBANI KWA LUKUVI KARIMJEE. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili tayari kuwaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu William Vangimembe Lukuvi leo Machi 28, 2026 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.