RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI MAALUM WA PEMBE YA AFRIKA NÀ BAHARI NYEKUNDU

RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI MAALUM WA PEMBE YA AFRIKA NÀ BAHARI NYEKUNDU
RAIS Mstaafu Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika kwa Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, jukumu linalomrejesha katika mstari wa mbele wa diplomasia ya bara Afrika. Uteuzi huo ulitangazwa na Mahmoud Ali Youssouf, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, ambaye alionesha imani kubwa katika uzoefu na uongozi wa Kikwete kushughulikia changamoto tata za kisiasa, amani na usalama katika ukanda huo. Ukanda huo unaendelea kuwa na changamoto nyingi, kuanzia migogoro ya kisiasa hadi maslahi ya kimkakati ya kimataifa, hasa kutokana na umuhimu wa Bahari Nyekundu katika biashara ya dunia.  Ni eneo ambalo si tu linahusu nchi za Afrika, bali pia lina mvuto wa nguvu za kimataifa. Katika nafasi hiyo mpya, Kikwete anatarajiwa kusaidia Tume hiyo  kuimarisha juhudi za kuleta amani kupitia diplomasia ya kuzuia migogoro, kukuza mazungumzo jumuishi, na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau mbalimbali. Aidha, alikabidhiwa jukumu la kuratibu juhudi za taasisi mbali…