RAIS DKT. MWINYI :“UONGOZI NA UDHAMINI BORA VITABADILISHA MICHEZO ZANZIBAR ”
RAIS DKT. MWINYI :“UONGOZI NA UDHAMINI BORA VITABADILISHA MICHEZO ZANZIBAR ”
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuimarisha miundombinu ya viwanja vya michezo na akademia za michezo ili kuinua sekta ya hiyo nchini. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 20 Machi 2026, alipokutana na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha kutoka Taasisi ya Tanzania Securities Limited, iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Ndg. George Shumbusho, waliofika Ikulu, Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi ameihakikishia taasisi hiyo kuwa Serikali itashirikiana nayo ili wazo lao la kukuza mpira wa miguu, ikiwemo kuongeza thamani ya vilabu, kuboresha maslahi ya wachezaji na kuwajengea mazingira ya kutambua thamani yao, linafanikiwa, kwani litatoa suluhisho la changamoto zilizopo katika sekta ya michezo. Aidha, ameishauri Tanzania Securities Limited kuweka mkazo zai…