OPERESHENI MBINGA DC: KASHUSHURA AANZA NA WALIMU WA HISABATI KUINUA TAALUMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Joseph Kashshura Rwiza,akizungumza katika baraza la Madiwani ambapo alisisitiza kuhusu madiwani kushirikiana na watendaji wa vijiji na walimu katika kuinua kiwango cha taaluma mashuleni. …………. Na Muhidin Amri, Mbinga HALMASHAURI  ya Wilaya Mbinga Mkoa wa Ruvuma, imeweka mikakati ya  kuinua kiwango cha ufaulu na kuboresha ufundishaji, ujifunzaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari. Miongoni  mwa  mikakati iliyowekwa ni pamoja na kufanya mitihani tembezi, kuendesha vikao vya walimu wa masomo, wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu kata ili kujadili mbinu bora za kuboresha ufaulu wa wanafunzi. Aidha Halmashauri hiyo imepanga kufanya tathmini ya kila mtihani ambayo itafanyika katika ngazi za shule, kata na Halmashauri ili kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi mapema pamoja na kuimarisha ufundishaji kuanzia elimu ya awali, shule za msingi hadi sekondari kwa kusimamia ukamilis…