OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA JIJI LA DAR ES SALAAM ZAKUBALIANA KUANDAA MAKUBALIANO KUANZIA KITUO CHA KUMBUKUMBU ZA MUUNGANO

OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA JIJI LA DAR ES SALAAM ZAKUBALIANA KUANDAA MAKUBALIANO KUANZIA KITUO CHA KUMBUKUMBU ZA MUUNGANO
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi. Cesilia Nkwamu akiwasilisha maelezo kuhusu andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi) wakati wa kikao baina ya wataalamu kutoka Ofisi hiyo, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam. ************** Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zimekubaliana kuandaa Hati ya Makubaliano (MoU) kwa ajili ya kuufanya Ukumbi wa Karimjee kuwa Sehemu ya Kituo cha Kutunza Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi). Akizungumza katika kikao baina ya wataalamu wa Ofisi hizo Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohammed Salum amesema makubaliano hayo ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Salum amesema O…