NIMEZINDUA MADARASA YATAKAYO ONDOA MSONGAMANO WA WANAFUNZI - PROF. SHEMDOE
NIMEZINDUA MADARASA YATAKAYO ONDOA MSONGAMANO WA WANAFUNZI - PROF. SHEMDOE
Na OWM - TAMISEMI, Bumbuli Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM -TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa amezindua madarasa matatu katika Shule ya Sekondari Kilivicha wilayani Bumbuli ambayo yataondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani, uliokuwa ukiikabili shule hiyo kwa muda mrefu. Prof. Shemdoe ameongeza kuwa madarasa hayo pia ni sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2028 ambao watakuwa wamehitimu darasa ya sita na la saba kwa pamoja na kutakiwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na mabadaliko ya mtaala mpya wa elimu unaotekelezwa na Serikali. Prof. Shemdoe amesema hayo leo Machi 21, 2026 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa madarasa hayo matatu yaliyojengwa kwa ufadhiri wa taasisi ya VUGA DELOPMENT INITIATIVE kwa gharama ya Shilingi Milioni 84,086,600/=. “Ni ukweli usiopingika kwamba, ujenzi wa madarasa haya utaondoa msongamano wa wanafunzi madarasani na ni maandalizi ya kupokea wana…