NEMC KUADHIMISHA SIKU YA “TAKA SIFURI”, YAHAMASISHA TAKA KUWA FURSA YA KIUCHUMI
NEMC KUADHIMISHA SIKU YA “TAKA SIFURI”, YAHAMASISHA TAKA KUWA FURSA YA KIUCHUMI
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wadau wa mazingira, linatarajia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Taka “Taka Sifuri” kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mbinu za kubadilisha taka kuwa malighafi au bidhaa nyingine, hatua inayolenga kuifanya taka kuwa fursa ya kiuchumi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 24, 2026, Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria wa NEMC, Hamadi Kissiwa, amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Machi 28 hadi Machi 30, 2026 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Amesema kaulimbiu ya kimataifa ya maadhimisho hayo ni “Wezesha taka sifuri kwenye sekta ya chakula”, huku kaulimbiu ya kitaifa ikiwa ni “Taka ni Fursa”. Ameongeza kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni. Kissiwa amefafanua kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kubadilisha mtaz…