NAIBU WAZIRI DUGANGE ASHIRIKI MAZISHI YA LUKUVI IDODI IRINGA
NAIBU WAZIRI DUGANGE ASHIRIKI MAZISHI YA LUKUVI IDODI IRINGA Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange (wa tatu kulia) akiwa na viongozi mbalimbali katika Kijiji cha Idodi, mkoani Iringa, kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi. Kushoto ni Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab Katimba na Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile. Mazishi hayo yamefanyika leo, Machi 31, 2026, nyumbani kwake Idodi, katika eneo la makaburi ya familia ambapo viongozi, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki wamejitokeza kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.