MWANAMKE AUAWA KWA SHAMBULIO LA MME, TUHUMA ZA MAPENZI NA JAMAA ALIYEMTAMBULISHA 'NI NDUGU'
MWANAMKE AUAWA KWA SHAMBULIO LA MME, TUHUMA ZA MAPENZI NA JAMAA ALIYEMTAMBULISHA 'NI NDUGU'
Mwanamke aitwaye Mariam Cosmas Mafumba (40), mkazi wa Kijiji cha Songambele, Kata ya Salawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amefariki dunia kufuatia kile kinachodaiwa kuwa ni shambulio kutoka kwa mume wake, likihusishwa na wivu wa mapenzi. Tukio hilo limegundulika Jumatatu, Machi 23, 2026 majira ya saa moja asubuhi, ambapo mwanamke huyo alikutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake katika mazingira ya kutatanisha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu alipigwa kwa kitu kigumu sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kichwani, kabla ya kupoteza maisha. Ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kinahisiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alimshuku Mariam kuwa na mahusiano na wanaume wengine. Kamanda Magomi amelielezea tukio hilo kuwa ni la kikatili na kusema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina…