MTI MMOJA, ENEO AMBALO SIMBA HULITUMIA KWA HONEYMOON KRETA YA NGORONGORO.
MTI MMOJA, ENEO AMBALO SIMBA HULITUMIA KWA HONEYMOON KRETA YA NGORONGORO.
Unaweza kustaajabu lakini ukweli upo hivyo, ukitaka kuwaona simba wakiwa katika harakati za kuongeza familia fika katika Kasoko ya Ngorongoro eneo la mti mmoja ambalo limezungukwa na vichaka, miti na nyasi za wastani. Eneo hili ni maarufu sana kwa waongoza utalii kutokana na makundi ya simba waliopo katika hifadhi hiyo kupenda kupumzika na hasa wanapokuwa katika msimu wao wa kujamiina ama kutafuta watoto na kuongeza familia. Simba hupenda kujamiiana mara baada ya kushiba ambapo zoezi hilo linafanyika mda wowote mchana au usiku. Tofauti na Binadamu ambapo Kazi Ngumu hufanywa na wanaume, kwa Simba ni tofauti, kazi ya kutafuta chakula ama Mawindo kwa ajili ya msosi wa familia huongozwa na simba jike ambapo mara baada ya kuhisi njaa na tamaa ya kujamiina huamua kutafuta chakula ili kwanza kushiba halafu kuingia kwenye harakati ya kuongeza familia. Wakati wa mawindo simba huchagua chakula cha kushiba na hapa ina maana simba hahangaiki sana na wanyama wadogo wadogo kama swala kwani kwake ni k…