Mradi wa CookFund unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na UNCDF waleta Mageuzi ya matumizi ya Nishati katika taasisi za umma.
Mradi wa CookFund unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na UNCDF waleta Mageuzi ya matumizi ya Nishati katika taasisi za umma.
Dar es Salaam, Tanzania Zaidi ya wanafunzi 62,000 kote Tanzania sasa wananufaika na majiko salama na safi zaidi kufuatia usakinishaji wa zaidi ya majiko ya kisasa 170 ya nishati safi ya kupikia katika shule na taasisi za umma zaidi ya 45. Hatua hii muhimu iliadhimishwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, ikionesha mchango wa mpango huu katika kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kukabiliana na ukataji wa miti. Mpango huu unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kupitia programu ya CookFund. Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Salome Makamba alisema: “Mapinduzi haya kuelekea matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kipaumbele cha kimkakati cha taifa kinachochangia kulinda mazingira, kuboresha afya ya umma na kuongeza ufanisi wa kiuchumi. Kwa kuzipatia shule na taasisi za umma teknolojia …