Mradi wa CERC waleta tabasamu Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mradi wa CERC waleta tabasamu Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Zege la Gagi linalojengwa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kupitia Mfuko wa Dharura (CERC) limeondoa adha ya usafiri iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu wananchi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani. Daraja hilo lenye urefu wa mita 11.2 na upana mita 8.2 linajengwa kwenye barabara ya Gagi ambalo linaunganisha Kata za Ndembezi na Ngokolo katika Manispaa hiyo. Akizungumza kwenye mahojiano maalum katika ziara ya kutembelea mradi huo, Diwani wa Kata ya Ndembezi na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Upendo John Sawa amesema kukosekana kwa daraja hilo ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa Kata hiyo kutokana na ugumu wa kupita katika eneo hilo hasa kipindi cha masika kutokana na kivuko cha awali kusombwa na maji. "kipindi cha masika akina mama walikuwa wanajifungulia hapa, wanafunzi kwenda shule mpaka wapatikane watu wa kuwavusha, wengine wanavushwa kwa pesa, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na wajumbe wake walikuwa wanakaa hapa kusubiri kuwavusha wa…