MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR--UFUNGUZI WA KONGAMANO LA TANO LA IDHAA YA KISHWAHILI--AICC--JIJINI ARUSHA
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR--UFUNGUZI WA KONGAMANO LA TANO LA IDHAA YA KISHWAHILI--AICC--JIJINI ARUSHA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Viongozi wa Serikali, Wadau wa Habari na wataalamu wa Lugha ya kiswahili katika ufunguzi wa Kongamano la Tano ( 5 ) la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha ( AICC ), Jijini Arusha . Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuunga mkono juhudi za kuikuza na kuieneza lugha ya kiswahili ili iendelee kutumika Duniani kote. Yameelezwa hayo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ufunguzi wa kongamano la Tano ( 5 ) la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Jijini Arusha. Akizungumza na viongozi wa serikali, wadau wa habari na wataalamu wa lugha ya kiswahili waliohudhuria katika Kongamano hilo, Mhe. Hemed amesema katika kufikia malengo ya kuifanya lugha ya Kiswahili kutumika duniani kote, Serikali zote mbili zitahakikisha zinaimari…