MAGEUZI YA SOKO LA KILIMO: TPHPA YAFUNGUA MILANGO YA TRILIONI 15 DUNIANI

MAGEUZI YA SOKO LA KILIMO: TPHPA YAFUNGUA MILANGO YA TRILIONI 15 DUNIANI
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imepiga hatua kubwa katika kuimarisha uchumi wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji wa masoko ya mazao ya kilimo nje ya nchi, hatua inayochochea ukuaji wa biashara ya kimataifa.  Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020/21 hadi 2023/24, mamlaka hiyo imefanikisha usafirishaji wa zaidi ya tani milioni sita za mazao mbalimbali yakiwemo mbogamboga, nafaka, matunda, na maua kwenda katika masoko ya kikanda na kimataifa.  Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, amebainisha kuwa thamani ya mauzo hayo imefikia dola za Marekani bilioni 6.6, kiasi ambacho ni sawa na takriban Shilingi trilioni 15.6 za Kitanzania, kikiakisi ufanisi wa mifumo ya ukaguzi na udhibiti mipakani. Ongezeko la thamani ya mauzo limekuwa la kuridhisha ambapo katika mwaka wa fedha 2023/24 pekee, Tanzania ilisafirisha tani milioni 3.5 nje ya nchi zenye thamani ya dola bilioni 3.54, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 25.4 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.  Mafanikio haya yam…