MADHARA YA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA DAWA: KIVURI KINACHONYEMELEA KIMYA KIMYA

MADHARA YA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA DAWA: KIVURI KINACHONYEMELEA KIMYA KIMYA
Rebecca John mkazi wa mtaa wa Majengo Kata ya Kishapu wilayani ya Kishapu mkoani Shinyanga Kila alfajiri, anapambana. Anaamka kabla ya jogoo kuwika, akijipanga kwenda kutafuta riziki ili familia yake ipate chakula, ada, na matumaini ya kesho. Lakini katika mbio hizi zisizo na pumziko, jambo moja muhimu hubaki nyuma—afya yake na ya familia yake. Na pale ugonjwa unapogonga, suluhisho la haraka huwa ni kununua dawa dukani bila ushauri wa daktari. Wengi huona ni njia ya kuokoa muda na gharama—bila kujua wanacheza na hatima ya maisha yao. Karibu katika malaka hii inayohusu matumizi yasiyo sahihi ya dawa za hospitali na dawa za tiba ya asili, watu wengi wamekuwa wakitumia bila kupewa utaratibu na wataalamu wa afya hivyo kupelekea madhara kwenye maisha yao na hata vifo.                             Na Sumai Salum Simulizi ya Rebecca John mkazi wa mtaa wa Majengo Kata ya Kishapu wilayani ya Kishapu mkoani Shinyanga, ni ushuhuda mchungu wa kile kinachoweza kutokea. “Nilikuwa nikiona mwanangu mwenye …