MADAKTARI 30 KUTOKA CHINA KUTIBU BURE UBUNGO DAR ES SALAAM

MADAKTARI 30 KUTOKA CHINA KUTIBU BURE UBUNGO DAR ES SALAAM
***** Zaidi ya madaktari bingwa 30 kutoka China na Tanzania wanatarajiwa kuweka historia mpya ya huduma za afya jijini Dar es Salaam, kwa kuanzisha kambi maalum ya matibabu ya bure itakayodumu kwa siku mbili mfululizo, Machi 28 na 29, mwaka huu. Kambi hiyo itafanyika katika viwanja vya Kituo kikubwa cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki cha "EACLC East Africa Commercial Logistics Centre" (EACLC), ikiwa ni jitihada za pamoja za wadau wa afya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila gharama yoyote. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amewataka wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa hiyo adhimu ya kupimwa na kutibiwa bure. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando akimzungumza Jiji Dar es salaam. Msando alisisitiza kuwa huduma hizo zitatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi, akiwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawaleta watoto wao pamoja na watu wenye changamoto mbalimbali za kiafya. K…