HELP TO HELP YAWAJENGEA WANAWAKE NGUVU YA KIDIJITALI
HELP TO HELP YAWAJENGEA WANAWAKE NGUVU YA KIDIJITALI
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM TAASISI ya Help to Help East Africa imeendesha mafunzo ya siku 14 kwa wasichana 150 kutoka mikoa 20 nchini, ikiwa na lengo la kuwawezesha kupata ujuzi wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza ushindani wao katika soko la ajira. Mafunzo hayo yanawalenga zaidi wasichana waliopo vyuoni pamoja na waliohitimu masomo yao, ili kuwajengea uwezo wa kitaalamu unaohitajika katika ajira za kisasa. Tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2015, tayari umewafikia takribani vijana 11,000 nchini, wakiwemo wanafunzi wa vyuo na wahitimu. Akizungumza katika mafunzo hayo, Meneja wa Mradi wa taasisi hiyo, Epifania Muhagama, amesema mradi huo unalenga kuwasaidia wasichana wasio na ujuzi wa awali wa TEHAMA kwa kuwapatia maarifa muhimu kama uandishi wa ripoti, uchambuzi wa data, matumizi ya barua pepe, akili mnemba (AI), pamoja na matumizi ya kompyuta kwa ujumla. Amesema tafiti zinaonesha kuwa ushiriki wa wanawake katika soko la ajira bado uko chini, …