GGML Kili Challenge Yashiriki Maonesho ya Kilimanjaro Marathon 2026
GGML Kili Challenge Yashiriki Maonesho ya Kilimanjaro Marathon 2026
Moshi, Tanzania GGML Kili Challenge inayotekelezwa kupitia GGML Kili Trust, inashiriki Kilimanjaro Marathon 2026, maarufu kama “Mbio za Watu”, kupitia maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Ushirika, Moshi, yaliyoanza tarehe 20 na kuendelea hadi 22 Machi. GGML Kilimanjaro Challenge Against HIV/AIDS ni mpango wa kuhamasisha ushiriki wa wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya UKIMWI nchini. Kupitia GGML Kili Trust, rasilimali hukusanywa na kuelekezwa kwenye miradi inayonufaisha moja kwa moja watu wanaoishi na VVU pamoja na taasisi zinazowahudumia. Mwaka huu, Kili Trust imeanza kushirikiana kwa karibu zaidi na asasi za kiraia kutoka maeneo mbalimbali nchini zinazotekeleza programu za kusaidia watu walioathiriwa na VVU na UKIMWI, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kufikia watu wengi zaidi. Kupitia banda la GGML Kili Challenge, washiriki wa mbio na wageni wa maonesho wanapata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu GGML Kili Challenge, namna ya kushiriki, pamoja na miradi inayotekelezwa chin…