ETDCO YATEKELEZA MRADI WA UMEME WA BILIONI 4.6 MTWARA

ETDCO YATEKELEZA MRADI WA UMEME WA BILIONI 4.6 MTWARA
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) wakipeana maelekezo ya  utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa laini maalum ya kusafirisha umeme kutoka Wilaya ya Masasi hadi Newala Mkoani Mtwara. ………….. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), imetenga shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa laini maalum ya kusambaza umeme ya msongo wa kilovolti 33 kutoka Wilaya ya Masasi hadi Newala Mkoani Mtwara. Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi wa ETDCO, Mhandisi Abdallah Mitenda, amesema kuwa mradi huo wenye urefu wa kilomita 76 kutoka Masasi hadi Newala utasaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii. Mhandisi Mitenda amesema kuwa wakazi wa Masasi na Newala watanufaika na mradi huo kwa kufanikisha shughuli mbalimbali za kiuchumi, …