BMH Kuadhimisha Miaka 10 kwa Harambee ya Bilioni 7 Kuboresha Huduma za Upandikizaji Uloto na Figo
BMH Kuadhimisha Miaka 10 kwa Harambee ya Bilioni 7 Kuboresha Huduma za Upandikizaji Uloto na Figo
Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma, inatarajia kuhitimisha rasmi maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake kwa kufanya harambee maalum ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya upandikizaji uloto na figo kwa wananchi wenye uhitaji. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi, amesema kuwa maadhimisho hayo yalianza Oktoba 13, 2025, na yatahitimishwa Mei 8, 2026, baada ya kudumu kwa takribani miezi saba. Prof. Makubi amesema kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuhamasisha wadau kushiriki katika harambee itakayolenga kukusanya shilingi bilioni 7 ndani ya kipindi cha miaka miwili. Fedha hizo zitatumika kusaidia matibabu ya wagonjwa 100, ambapo 50 ni watoto wenye ugonjwa wa selimundu wanaohitaji upandikizaji wa uloto, na wengine 50 ni wagonjwa wa figo. Ameeleza kuwa gharama za matibabu hayo ni kubwa, hivyo hospitali imeona umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo …