πππππππππ ππππ ππππππ πππ ππππ πππππ ππ πππππππ ππππππππππ ππππ Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia akizungumza na waandishi wa habari …….. Zimesalia siku chache kabla ya kufikiwa kwa ukomo wa usajili wa hiari kwa taasisi zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi nchini. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetangaza kuwa ifikapo tarehe 9 Aprili mwaka huu, itaanza kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo faini ya hadi shilingi bilioni tano kwa taasisi zitakazokiuka taratibu hizo. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) leo Machi 26, 2026 imetoa msisitizo wa mwisho kwa taasisi zote za umma na binafsi nchini, ikizikumbusha kuwa muda wa usajili wa hiari unafikia tamati tarehe 8 Aprili, 2026. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, amesema kuwa serikali imetoa muda wa kutosha tangu mwaka 2024 ili kutoa fursa kwa taasisi kujipanga. “Serikali ilitoa muda wa kutosha wa kujisajili. Muda huo ulianza Aprili 2024 wakati Rais wa Jamhuri …