WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA MIGOGORO YA ARDHI
-Awasisitiza watendaji kuwafuata wananchi na kutatua kero zinazowakabili WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasisitiza Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na watumishi wa umma wahakikishe wanatenga muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hususani kwenye migogoro ya ardhi katika ngazi zao za kiutawala. Ameyasema hayo leo Ijumaa, Februari 6, 2026 wakati wa kuahirisha Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 jijini Dodoma, akisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwafuata wananchi, kuwasikiliza na kuchukua hatua za haraka za kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakiwa katika maeneo yao. “Wafuateni, wasikilizeni na tatueni kero zao ili wasilazimike kwenda ngazi za juu au kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa kwa masuala ambayo mngeweza kuyafanyia kazi.” Waziri Mkuu ameongeza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona wananchi wakihudumiwa ipasavyo. Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuhakikisha ku…