WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA UCHUNGUZI KUCHOCHEA UWAJIBIKAJI NA MABORESHO YA SERA
WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA UCHUNGUZI KUCHOCHEA UWAJIBIKAJI NA MABORESHO YA SERA
Na Bora Mustafa,Arusha. Waandishi wa habari za mazingira Kanda ya Kaskazini na Kati wametakiwa kuandika habari za uchunguzi zitakazochochea mabadiliko ya sera na sheria pamoja na kuhimiza uwajibikaji katika jamii. Wito huo umetolewa wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari za mazingira yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanahabari Inayosaidia Jamii za Asili (MAIPAC), yaliyofanyika jijini Arusha. Akitoa mada katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema kuwa katika uandishi wa kisasa, waandishi wanapaswa kujikita zaidi kwenye habari za uchunguzi badala ya kuandika habari za matukio ya kila siku. Amesema kuwa lengo la uandishi wa habari linapaswa kuwa kuchochea mabadiliko ya sera na sheria, lakini pia kuibua uwajibikaji kwa wadau mbalimbali. “Mafunzo haya yameandaliwa ili waandishi muandike habari za uchunguzi za mazingira zitakazochochea mabadiliko ya …