TUSIWAFICHE FAMILIA MALI ZETU
Katika jamii zetu kumekuwa na desturi ya baadhi ya watu kuamini kuwa ni vizuri kuwa na mali fiche ambazo hazijulikani na mwenzi (mke au mume), watoto, au hata ndugu wa damu. Desturi hii imeanza kujengeka zaidi kwa baadhi ya wanaume kuficha au kufanya miradi kwa siri bila kushirikisha familia, hasa wake na watoto. Hali hii imekuwa ikisababisha kupotea kwa mali, hasa pale kunapotokea kifo cha ghafla cha mhusika. FAIDA ZA KUTOFICHA MALI NA KUSHIRIKISHA FAMILIA Familia hunufaika na urithi halali Hupunguza au kuzuia migogoro ya kifamilia na kijamii Huleta mwendelezo mzuri wa mali kwa vizazi vijavyo Husaidia kuimarisha uchumi wa familia HASARA ZA KUFICHA MALI AU KUWEKA MIRADI FICHE Kwa utafiti mdogo nilioufanya maeneo yangu ya kazi na mtaani, nimebaini kuwa kuna watu wengi, hususan wanaume wanaoishi maeneo ya mijini, wana desturi ya kuwa na miradi ambayo familia zao hazijui. Mfano, mtu hununua kiwanja kwa siri au kujenga nyumba bila familia kufahamu. Desturi hii ina hasara kubwa, zikiwemo: Familia ku…