TABESA YAZINDUA ‘SAUTI APP ’ KURAHISISHA MAWASILIANO KWA WENYE CHANGAMOTO YA KUSIKIA
TABESA YAZINDUA ‘SAUTI APP ’ KURAHISISHA MAWASILIANO KWA WENYE CHANGAMOTO YA KUSIKIA
MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Jocelyne Joshua, amesema wao kama kikundi cha Tanzania Biomedical Engineering Students Association (TABESA) wamebuni teknolojia maalum itakayowawezesha watu wenye changamoto ya usikivu kujumuika kikamilifu katika jamii na kueleweka kwa urahisi. Jocelyne ambaye anasomea ya Shahada ya Uhandisi Tiba amesema awali waliamini kuwa watu wenye changamoto ya usikivu ni lazima wawe na msaidizi wa pembeni kwa ajili ya kutafsiri lugha za alama, lakini uhalisia ni kwamba wasaidizi hao ni wachache sana hali inayowafanya wahusika kukutana na watu wengi wasioweza kuwasiliana nao kwa lugha ya alama. Amesema bunifu hiyo imekuja na application yenye uwezo wa kubadili alama za vidole na kuzipeleka moja kwa moja katika maneno na sauti ili kusaidia katika mawasiliano. “Kwa mfano, walimu wanaofundisha watoto wenye changamoto hizi inapaswa wawe wanazijua lugha za alama au wawe na mtu wa pembeni atakayewasaidia kuwael…