SHIRIKA LA KIVULINI LAZINDUA MRADI WA KUTOKOMEZA UKEKETAJI TARIME MKOANI MARA
SHIRIKA LA KIVULINI LAZINDUA MRADI WA KUTOKOMEZA UKEKETAJI TARIME MKOANI MARA
Shirika la kutetea haki za wanawake la KIVULINI limezindua Mradi wa Kutokomeza Ukeketaji na Ndoa za Utotoni uitwao 'My Body, My Life', utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka huu 2026 katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara. Shirika hilo lenye ofisi kuu jijini Mwanza linatekeleza mradi huo kwa upande wa Tanzania huku nchini Kenya ukitekelezwa na mashirika mawili ambayo ni KAKENYA'S DREAM na MICONTRAP kwa ufadhili wa shirika la FOKUS kutoka nchini Norway. Uzinduzi huo umefanyika Ijumaa Februari 06, 2026 katika shule ya sekondari ya wasichana Borega wilayani Tarime ukiambatana na Madhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji yenye kaulimbiu isemayo, Sauti Yetu, Tokomeza Ukeketaji. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema makundi mbalimbali ikiwemo mabinti walio shule na nje ya shule, waalimu, wazazi, maafisa maendeleo ya jamii, maafisa ustawi wa jamii, viongozi wa dawati la jinsia, viongozi wa Vijiji na Kat…