SERIKALI YASISITIZA UWEKEZAJI MIUNDOMBINU NA USALAMA WA KIDIGITALI
SERIKALI YASISITIZA UWEKEZAJI MIUNDOMBINU NA USALAMA WA KIDIGITALI Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb), amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ya TEHAMA ikiwemo minara, nyaya za mawasiliano, satelaiti na vituo vya data, ili kukuza sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari nchini. Akizungumza Februari 26, 2026 katika kikao kazi kati ya Wizara na wadau wa Sekta Binafsi kilichofanyika katika viwanja vya Wizara, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, amesema kuwa sambamba na uwekezaji huo, ni muhimu kuweka mkazo katika ulinzi na usalama wa kidigitali ili kulinda miundombinu dhidi ya vitisho vya kimtandao. Aidha amebainisha kuwa hatua zinazotarajiwa kuhusiana na uanzishwaji wa akaunti ya Kidigitali ya Uchumi na Maendeleo ya Mkakati wa Uchumi wa Kidigitali zinatoa mwanga wa hatua za baadaye za utekelezaji, hivyo ni lazima kuweka kipaumbele katika utekelezaji wake kwa wakati. Pia ameongeza kuwa Serikali inaendelea kujipanga kukamilisha na kut…