SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUANZISHA MFUMO WA SOKO LA AJIRA KIDIJITALI
SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUANZISHA MFUMO WA SOKO LA AJIRA KIDIJITALI Na. OWM – KAM (Dar es salaam) Waajiri kutoka Sekta Binafsi wamefurahishwa na kuipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Wazifri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kuanzisha Mfumo wa Taifa wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira (NLMIS) wakieleza kuwa hatua hiyo ni mageuzi makubwa katika usimamizi na upatikanaji wa taarifa sahihi za Ajira nchini. Wamesema mfumo huo utawarahisishia kupata takwimu na taarifa za Ajira zinazozalishwa kwa haraka na kwa wakati, hivyo kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu mahitaji ya rasilimali watu kulingana na mwelekeo wa soko. Akizungumza Februari 25, 2026, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa Power Group Technologies Tanzania Limited Salha Irando, amesema Mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika uandaaji wa mikakati na mipango inayohusu taarifa za soko la ajira kwa usahihi na ufanisi . Naye, Mkuu wa Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Bakharesa Group Francis Ndenje amesema mfumo huo utasaidia katika upatikanaji wa takwimu sahihi na za wakati utaka…