Posts

SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED SASA YAENDA HADI NGAZI YA SHAHADA YA UZAMILI (MASTERS)

SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED SASA YAENDA HADI NGAZI YA SHAHADA YA UZAMILI (MASTERS)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Adolph Mkenda afungua mlango wa mazungumzo kwa Taasisi na Makampuni mbalimbali kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia kusomesha Wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kutoka ngazi ya awali ya kidato cha sita hadi ngazi ya Shahada ya Uzamili kwani Wizara imejipanga vizuri kuhakikisha fedha watakazotoa zinakwenda mahali panapotakiwa Waziri Mkenda ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Februari 25,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kutolewa kwa ufadhili huo na Wanafunzi kuripoti katika Vyuo husika. Ambapo amesema kuwa tayari walishapanga kutoa ufadhili katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na kwa kuanza waliamua kupeleka Wanafunzi katika Vyuo viwili vya hapa nchini cha Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha na kampasi ya Indian Institute of Teknoloji kilichopo Zanzibar ambavyo vyote vimejikita katika masuala ya Sayansi.  Na kuongeza kuwa tayari Wanafunzi wamesharipoti katika Chuo cha Nelson Mandel…