RC MBONI MHITA ATOA MAELEKEZO MAZITO KUIMARISHA ULINZI WA BARABARA, AIPONGEZA TANROADS NA TARURA KWA KAZI KUBWA
RC MBONI MHITA ATOA MAELEKEZO MAZITO KUIMARISHA ULINZI WA BARABARA, AIPONGEZA TANROADS NA TARURA KWA KAZI KUBWA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita a kizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita a kizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi, akitaka usimamizi mkali wa barabara na uwajibikaji wa viongozi katika ngazi zote. Akizungumza Februari 24, 2026 wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhita amesema pamoja na changamoto za kibajeti na athari za mabadiliko ya tabianchi, barabara nyingi zimeendelea kupitika mwaka mzima, jambo linalodhihirisha dhamira thabiti ya Serikali katika kuhakikisha miundombinu inakuwa endelevu. Amesema Serikali inaendelea kuelekeza rasilima…