RC MAKALLA AIPONGEZA AICC KWA HUDUMA YA UTALII WA MIKUTANO ARUSHA
RC MAKALLA AIPONGEZA AICC KWA HUDUMA YA UTALII WA MIKUTANO ARUSHA
Na Bora Mustafa,Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, ameipongeza Menejimenti na wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kwa mchango wao mkubwa katika kukuza utalii wa mikutano pamoja na kulitangaza taifa kimataifa. Makalla ametoa pongezi hizo Februari 6, 2026, wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Wafanyakazi wa AICC, akisema kituo hicho kimefanikiwa kuratibu mkutano wa kimataifa ulioshirikisha nchi zaidi ya 120 uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha. Pia amesema mafanikio hayo yanaonesha wazi kuwa AICC imejipanga kikamilifu kuhudumia Mkutano wa Bunge la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu jijini Arusha. Aidha Makalla amesema AICC imekuwa na mchango mkubwa katika kuutangaza Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla katika ramani ya kimataifa, akiwataka wafanyakazi wote wa kituo hicho kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maono na malengo ya Serikali. Amesisitiza umuhimu wa ku…