RABIA NA SENDIGA WASISITIZA BIMA YA AFYA KWA WOTE MANYARA

RABIA NA SENDIGA WASISITIZA BIMA YA AFYA KWA WOTE MANYARA
…………….. Na John Walter-MANYARA Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Rabia Abdallah Hamid, kwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga, wamewahimiza wananchi kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa uhakika. Wameyasema hayo wakati wakizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Gidahababieg, Wilaya ya Hanang, katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika mkoani Manyara. Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Rabia Abdallah Hamid amesema dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na uhakika wa kupata matibabu pindi anapokumbwa na dharura za kiafya kupitia mpango wa Bima ya Afya kwa Wote. Ameeleza kuwa ugonjwa haubishi hodi, hivyo kuwa na bima ya afya ni kinga muhimu kwa wananchi kwani huwapa uhakika wa matibabu wakati wowote bila changamoto za kifedha. Aidha amewahimiza wananchi kumuunga …