PPAA: Moduli Mpya Yaongeza Ufanisi katika Usimamizi wa Malalamiko na Rufaa za Ununuzi wa Umma
PPAA: Moduli Mpya Yaongeza Ufanisi katika Usimamizi wa Malalamiko na Rufaa za Ununuzi wa Umma
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema jumla ya malalamiko 549 (Administrative Reviews) yamewasilishwa na kushughulikiwa na Taasisi Nunuzi kupitia Moduli jambo linaloonyesha mwitikio chanya kutoka kwa wazabuni na Taasisi Nunuzi katika kutumia mfumo kwa ajili ya kupokea, kuchambua na kutoa maamuzi kuhusu malalamiko yanayohusu michakato ya ununuzi wa Umma. Jumla ya rufaa 26 zimewasilishwa na kushughulikiwa na Mamlaka ya Rufani kupitia moduli hiyo, hatua ambayo imeongeza ufanisi katika usimamizi wa rufaa, kupunguza muda wa kushughulikia mashauri, na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa haki. James Sando Katibu Mtendaji Mamlaka ya Rufani ya Wazabuni za Umma (PPAA) ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika Makutano na Waandishi wa Habari akitangaza miradi ya maendeleo na fursa za vijana kwa mwaka 2025/20. Sando amesema kwa ujumla, takwimu hizo zinaonesha mafanikio makubwa ya awali katika matumizi ya Moduli ya kushugulikia Malalamiko na Rufaa, zinaimarisha mifumo ya un…