OMO ahitimisha ziara kuwatembelea na kuwafariji Wananchi wanyonge
OMO ahitimisha ziara kuwatembelea na kuwafariji Wananchi wanyonge
Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman amesisitiza haja ya Viongozi kuwatembelea na kuwafariji Wananchi wanyonge, sambamba na kuziombea mafanikio juhudi za kuleta Maridhiano ya Kisiasa Zanzibar, zinazoendelea kati ya Upande wake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan. Mheshimiwa Othman ameeleza haja hiyo leo Alhamis Februari 26, 2026, akiwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kichama wa Mjini Unguja, kwa nyakati tofauti, alipoendelea kuwatembelea na kuwajulia-hali Wazee, Wagonjwa na pia Watu wanaokabiliwa na matatizo mbali mbali ya kijamii wakiwemo Wafiwa na Wasiojiweza. Amesema, kwa-mujibu wa taarifa za hivi punde amearifiwa na 'upande wa pili' kuwa wameketi kujadili juhudi za kuleta Maridhiano ya Kisiasa Nchini, na 'wamefikia pema', bali la muhimu zaidi ni kwa kila mmoja kuzidisha Dua, ili kuombea Mustakabali Mwema wa Mazungumzo yanayoendelea baina ya Vyama hivyo Vikuu vya Kisiasa, na Taifa kwa ujumla. "Muhi…