MWANAFUNZI MUHAS ABUNI KIFAA CHA KUPIMA MANJANO BILA KUCHUKUA DAMU.

MWANAFUNZI MUHAS ABUNI KIFAA CHA KUPIMA MANJANO BILA KUCHUKUA DAMU.
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv MWANAFUNZI wa Uhandisi Tiba kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wamekuja na ubunifu wa kifaa kinachoitwa BiliMeasure, kinachotumika kupima kiwango cha bilirubini inayosababisha homa ya manjano kwa watoto wachanga bila kuchukua sampuli ya damu. Akizungumza katika Maonesho ya Pili ya Ubunifu ya MUHAS (Innovation Week 2026), yaliyofanyika leo Februaria 24, 2026 jijini Dar es Salaam mwanafunzi wa Uhandisi Tiba, Abubakar Mathias, alisema zaidi ya asilimia 60 ya watoto huzaliwa wakiwa na homa ya manjano, hali inayowalazimu kupelekwa kwenye kifaa maalumu cha tiba ya mwanga (phototherapy) kwa matibabu. Alisema kifaa hicho kitafanya kazi sambamba na phototherapy kwa kupima maendeleo ya matibabu ya mtoto anayeugua manjano. Kifaa hicho huvalishwa mtoto kifuani au kichwani wakati wa matibabu na hupima kiwango cha bilirubini papo kwa papo bila maumivu. “Kwa sasa vipimo vya manjano hutegemea sampuli ya damu, hali inayosababisha maumivu kwa watoto w…