MIAKA 30 YA OCEAN ROAD ILIVYOFUFUA MATUMAINI YA KUISHI KWA MAMILIONI YA WATU

MIAKA 30 YA OCEAN ROAD ILIVYOFUFUA MATUMAINI YA KUISHI KWA MAMILIONI YA WATU
NI miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Saratani nchini Tanzania (Ocean Road). Kuanzishwa kwake kumeleta matumaini ya kuendelea kuishi kwa mamilioni ya wananchi. Kila safari kubwa huanza na maono, matumaini, ujasiri na imani kwamba hata katika nyakati ngumu maisha yanaweza kulindwa. Mwaka 1996, katika changamoto za kiafya na rasilimali chache, wazo moja lilizaliwa si kwa hofu bali kwa maarifa, huruma na uthubutu. Haikuwa rahisi kuanza safari hiyo ngumu, lakini taasisi hiyo ilijengwa kwa dhamira thabiti ya kuhudumia watu. Dkt. Hamza Maunda anasimulia kuwa hali ilikuwa ngumu kwa kuwa taasisi ilianza ikiwa na uhaba wa wafanyakazi na vifaa tiba kwa ajili ya matibabu ya saratani. “Taasisi hiyo iliendelea kuimarika siku hadi siku mpaka kufikia hatua ya kuwa na wataalamu waliosoma ndani ya taasisi hiyo,” alisema. “Pamoja na changamoto zote, tuliweza kujijenga siku hadi siku, na mwaka 2013 taasisi ilianzisha masomo ya kuwafundisha madaktari kubobea katika eneo la saratani; hiyo ilikuwa hatua m…