MAMLAKA YA RUFANI YAIMARISHA HAKI ZA WAZABUNI KUPITIA MFUMO WA KIDIJITALI NeST

MAMLAKA YA RUFANI YAIMARISHA HAKI ZA WAZABUNI KUPITIA MFUMO WA KIDIJITALI NeST
Na Dotto Kwilasa, Dodoma Katika kuimarisha uwazi na upatikanaji wa haki kwenye ununuzi wa umma, Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendelea kufanya mageuzi ya kidijitali kwa kuimarisha matumizi ya mfumo wa NeST unaowezesha wazabuni kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki. Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 25, 2026 jijini Dodoma, Katibu Mkuu Mtendaji wa Mamlaka hiyo, James Sando, amesema mfumo huo umeunganisha taasisi zote nunuzi nchini, hatua inayomruhusu mzabuni kuwasilisha rufaa yake kwa haraka, kwa uwazi na bila urasimu. Amesema kupitia mfumo huo, Mamlaka ina uwezo wa kufuatilia nyaraka zote zinazohusiana na zabuni inayolalamikiwa, jambo linalosaidia kufanya maamuzi yenye haki kwa kuzingatia vielelezo halisi. Katika kuhakikisha mfumo huo unatumika ipasavyo, Sando amesema Mamlaka imekuwa ikitoa mafunzo ya matumizi ya moduli ya malalamiko na rufaa kwa wadau wa ununuzi wa umma, hususan vijana na makundi maalum, ili kuwajengea uelewa wa taratibu za…