MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI HAFLA YA KUSIMIKWA KWA UONGOZI WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE TANZANIA

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI HAFLA YA KUSIMIKWA KWA UONGOZI WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE TANZANIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Viongozi wa Dini wana wajibu wa pekee wa kuliombea Taifa kama ambavyo Biblia Takatifu ilivyoelekeza.  Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026. Amewahimiza kuendelea kumuombea afya njema,busara na hekima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ndiye kiongozi Mkuu wa Nchi na kupitia yeye nchi itaendelea kuwa salama. Amewataka Viongozi hao kutambua wanapaswa kutimiza wajibu na kuwa na moyo wa utumishi kwa nchi, waumini na Kanisa kwa ujumla. Halikadhalika, Makamu wa Rais amewahimiza Viongozi wa Dini kutambua wajibu wa kulinda mazingira kwa kuendeleza jitihada za uhifadhi mazingira na kuwafundisha waumini kujiepusha na ukataji miti, uchomaj…