KIVUMBI TAMASHA LA AMANI NA MAENDELEO KISHAPU

KIVUMBI TAMASHA LA AMANI NA MAENDELEO KISHAPU
Na Sumai Salum- Kishapu Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imewaka moto wa michezo kufuatia kuendelea kwa Tamasha la Amani na Maendeleo linalofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Buduhe. Tamasha hilo lililoanza rasmi Februari 23, 2026 linatarajiwa kuhitimishwa Februari 28, 2026, likiwa limekusanya mamia ya washiriki na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Katika mchezo wa dakika 90 uliopigwa leo, timu ya Kishapu Veteran imeonyesha ubabe kwa kuichapa Mafundi FC mabao 4-0, ushindi uliotikisa tamasha na kuacha mashabiki wakishangilia kwa nderemo na vifijo huku Mafundi FC, msumeno wao leo haukukata kama ilivyotarajiwa, mshambuliaji Benjamini akiipa timu yake bao 1 la kufutia machozi. Wafungaji wa Kishapu Veteran ni Lupatiko (magoli 2), Santos (goli 1) na Sheby (goli 1). Ushindi huo umeifanya Kishapu Veteran kuvuna pointi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania taji la tamasha hilo. Tamasha hilo limeendelea pia kushuhudia michezo mingine yenye ushindani mkali huk…