IAA YAENDELEA KUTOA WAHITIMU WENYE KUCHOCHEA MABADILIKO CHANYA KATIKA JAMII
IAA YAENDELEA KUTOA WAHITIMU WENYE KUCHOCHEA MABADILIKO CHANYA KATIKA JAMII
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimeendelea kutoa wahitimu mahiri wenye ujuzi wa kitaaluma, maadili na uwezo wa kiuongozi, wenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika taasisi na jamii wanazozihudumia. Akizungumza Februari 6, 2026, wakati wa mahafali ya 27 ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya mwaka 2025 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha, Mkuu wa Chuo Profesa Eliamani Sedoyeka, amesema maboresho yanayoendelea katika huduma za ufundishaji na ujifunzaji yameiwezesha IAA kuandaa wataalamu wanaokidhi mahitaji ya taifa na soko la ajira. Prof. Sedoyeka amewasisitiza wahitimu kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu na uzalendo wanapotekeleza majukumu yao huku akiwataka kutumia ujuzi wa kisayansi, tafiti na maadili katika kufanya maamuzi katika maeneo watakayoaminiwa kuyahudumia. “Mmeandaliwa kuwa viongozi wenye maarifa, maadili na uwezo wa kuongoza mabadiliko chanya katika taasisi na jamii mnazozihudumia, Ni wajibu wenu kuzingatia uwajibikaji, uadilifu na uzalendo katika …