GF YAADHIMISHA MIAKA 19 YA KUANZISHWA KWAKE,ASILIMIA 90 YA WAFANYAKAZI NI WAZAWA.

GF YAADHIMISHA MIAKA 19 YA KUANZISHWA KWAKE,ASILIMIA 90 YA WAFANYAKAZI NI WAZAWA.
Katika kuadhimisha miaka 19 ya kuanzishwa kwa kiwanda cha kuunganisha magari cha GF, uongozi wa kiwanda hicho umesema unajivunia kuwa sehemu ya kuzalisha ajira, huku ukieleza kuwa asilimia 90 ya wafanyakazi wake ni wazawa. Akizungumza na waandishi wa habari, leo Februari 07, 2026, makao makuu ya kiwanda hicho yaliyopo Kibaha mkoani Pwani, Meneja Mkuu wa kiwanda cha GF, Ezra Mereng, amesema miaka 19 ya dira na matumaini yalianza kama ndoto, lakini hadi sasa kiwanda hicho kinajivunia kuzalisha magari ya aina mbalimbali. “Leo tunajivunia kusherehekea miaka 19 ya GF, na sisi kama kiwanda tunajivunia kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wafanyakazi ni vijana wazawa wa hapa Tanzania waliotoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini." Naye Meneja Chapa na Masoko wa GF Group, Salman Karmal  pamoja na kufurahia mafanikio ya kiwanda hicho, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za uwekezaji zinazowavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza …