Geita Kuimarisha Mapambano Dhidi ya VVU Miongoni mwa Wachimbaji Wadogo

Geita Kuimarisha Mapambano Dhidi ya VVU Miongoni mwa Wachimbaji Wadogo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt. Omary Sukari (aliesimama) akiongoza majadiliano wakati wa kikao kazi kilichokutana jijini Mwanza kupanga mikakati itakayotumika kufikisha huduma za VVU na UKIMWI kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita. Na Mwandishi Wetu WADAU mbalimbali wamekutana jijini Mwanza katika kikao kazi maalum chenye lengo la kuimarisha mwitikio wa VVU miongoni mwa wachimbaji wadogo mkoani Geita, hatua inayolenga kuongeza kasi ya kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Kikao hicho kimefanyika katika kipindi muhimu, ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Geita unakadiriwa kuwa na takriban asilimia 10 ya jumla ya wachimbaji wadogo milioni nne waliopo nchini Tanzania, wanaofanya kazi katika zaidi ya maeneo 100 ya uchimbaji. Licha ya kiwango cha maambukizi ya VVU mkoani Geita kwa ujumla kuwa asilimia 4.9, tafiti zinaonesha kuwa katika jamii za wachimbaji wadogo kiwango hicho kinakisiwa kufikia asilimia 9.3, karibu mara mbili ya wastani wa mkoa. Aidha, mko…