ZHC yamuaga Bi Mkubwa Sururu Shaaban
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC), Ndg. Sultan Said Suleiman, amewataka wafanyakazi wa Shirika hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uwajibikaji na uaminifu kwa kuiga mifano ya wafanyakazi waliotangulia ambao wameacha alama ya utendaji bora, sambamba na kuimarisha uzalendo na ushirikiano mahali pa kazi. Ndg. Sultan ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mfanyakazi wa Shirika la Nyumba aliyestaafu kutoka kada ya Masjala, Bi Mkubwa Sururu Shaaban, iliyofanyika katika Ofisi za ZHC, Darajani Zanzibar. Amesema Shirika litaendelea kuthamini na kutambua mchango wa Bi Mkubwa katika kipindi chote cha utumishi wake, akieleza kuwa jitihada zake zimekuwa sehemu ya chachu ya maendeleo na mafanikio ya Shirika. Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu alimkabidhi Bi Mkubwa zawadi maalum kama ishara ya upendo na shukrani kutoka kwa familia ya ZHC, zikiwemo pikipiki aina ya TVS kwa ajili ya shughuli za kujipatia kipato pamoja na vifaa vingine. Kwa upande wake, mstaafu Bi Mkubwa Sururu Shaa…